Juhudi zaidi zinapaswa kuwekwa ili kuhakikisha thuluthi mbili ya uwakilishi wa akina mama katika nafasi za uwongozi inaafikiwa humu nchini.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Wanawake ulimwenguni mama wa taifa Bi Margret Kenyata amesema akina mama wana uwezo mkubwa wa kufanikisha maendeleo nchini iwapo watawezeshwa
Aidha amewataka akina mama kusimama kidete na kuwania nafasi za uwongozi huku pia akisisitiza kwamba juhudi za pamoja zinahitajika kupigana na ukeketaji sawa na visa vya ndoa za mapema ili kufanisha ukuaji wa jamii ya kesho.