Muswada wa marekebisho ya katiba mwaka wa 2020 umewasilishwa kwenye Bunge la kitaifa na kusomwa kwa mara ya kwanza.
Spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi amethibitisha kupokea uamuzi wa mabunge 46 ya kaunti kuhusu BBI mabunge 43 yakipiga ndio na mabunge matatu yakipinga bbi kaunti ya uasin gishu ikisubiriwa kuamua ikiwa inaunga mkono au la.
Muturi amesema muswada huo wa BBI utakabidhiwa kamati za bunge kuhusu sheria kwenye bunge la Seneti na bunge la kitaifa ili kamati hizo ziandae vikao vya pamoja kujadili mswada huo
Hata hivyo amesema wananchi wamehusishwa kikamilifu katika mchakato mzima akisema na kwamba kama wabunge watahakikisha mswada huwo uanapasishwa bungeni.