Seneta wa Siaya ambaye pia ni kiongozi wa wachache katika bunge la seneti James Orengo amewataka wafanyikazi wa serikali kukoma kutumia muda wao mwingi katika maswala ya siasa na badala yake kuwatumikia wananchi
Orengo amewataka viongozi wote nchini kushirikiana na rais Uhuru Kenyata kuhakikisha mshikamano wa kitaifa kupitia ripoti ya upatanishi BBI.
Aidha ameongeza kuwa muda wa kufanya siasa haujafika na itakuwa vema iwapo ajenda za maendeleo zitapewa kipau mbele
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na gavana wa Machakos dakta Alfred Mutua akisema hatua ya viongozi wa kisiasa kurushiana cheche za maneno hadharani inatishia umoja wa kitaifa.
Kulingana na Mutua hakuna maendeleo ambayo inaweza kuafikiwa katika nchini yoyote ikiwa siasa ndo lugha ya pekee wanayojua wakenya kutoka kwa viongozi.