WAKAAZI WA NAREWA KAUNTI NDOGO YA TURKANA YA KATI WAPOKEA HUDUMA ZA MAJI BAADA YA KUPAZA KILIO CHAO KWA SERIKALI

  • Post category:County News

Baada ya wakaazi wa Narewa wadi ya Kanamkemer kaunti ndogo ya Turkana ya Kati kulalamikia uhaba wa maji katika eneo hilo sasa serikali kaunti ya Turkana imeanza zoezi la kusambaza maji kwa makaazi yao.

Akizungumza wakati wa zoezi la kusambaza maji katika eneo hilo mtawala wa wadi ya Kanamkemer Shaban Lotabo amesema wamehamua kusambaza maji kwa muda huu wa mapambano dhidi corona huku akidokeza kuwa wana mpango wa kupata suluhu  la kudumu kwenye suala la ukosefu wa maji katika eneo hilo.

Aidha Lotabo amesema wametumia fursa hiyo kutoa msaada  kwa familia zilizoathirika na janga la mafuriko lilokumba eneo hilo ambapo pia amewahakikishia wakaazi wa Narewaa usalama wao baada ya kuongezeka kwa visa vya ukosefu wa usalama.

Hata hivyo wakaazi wa Narewa wadi ya Kanamkemer,wamepongeza hatua ya serikali ya kaunti kusikia kilio chao kwa kuwapa maji wakati huu taifa linapambana na ugonjwa wa corona huku wakitoa wito kwa uongozi wa kaunti kuwakumbuka kila mara isiwe tu wakati wa majanga.

Robert Elim

Presenter and News Editor at North Rift Radio Kenya