Wauguzi katika kaunti ya Trans-Nzoia, hii leo wamepiga kambi nje ya lango la bunge la kaunti hiyo wakilalamikia kukosa mishahara kwa miezi mbili sasa
Wauguzi hao wanasema wamekuwa katika mgomo kwa miezi miwili, hii ni baada ya serikali ya kaunti kudinda kutia sahihi makubaliano ya kurejea kazi kama ilivyoagizwa na baraza la magavana nchini
Wauguzi hao sasa wanamtaka Gavana wa kaunti hiyo Patrick Khaemba kuingilia kati mara moja huku wakisisitiza kwamba watarejea kazini pindi tu maslahi yao yatakapoangaziwa.