WAHUDUMU WA KLINIKI KAUNTI YA TURKANA WAMEPOKEA MAFUNZO YA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA COVID-19

  • Post category:County News

Muungano wa maafisa wa kilinik kaunti ya turkana imetoa mafunzo kwa zaidi ya wahudumu 40 wa afya kaunti hii kuhusu jinsi ya kukabiliana na virusi vya corona iwapo vitaripotiwa.

Katibu mkuu wa Muungano wa Maafisa wa kliniki tawi la Turkana Joseph Chebii amesema mafunzo hayo ni moja ya mikakati ambayo serikali ya kaunti ya turkana imeweka kukabiliana na janga la corona.

 Aidha amepongeza ushirikiano uliopo baina ya wahudumu wa afya kaunti hiyo ambao umechangia kufanikisha mafunzo hayo huku   akitoa wito kwa wananchi kufuata maagizo ya serikali ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

Kwa upande wao wahudumu wa kliniki kaunti ya Turkana waliofaidi na mpango huo wamepongoze juhudi zilizowekwa na muungano huo wa wakuwapa mafunzo hayo kwani ujuzi ambao wamepata utawasaidia kujikinga dhidi ya virusi vya corona na pia kuwahudumia watu watakaoripotiwa kuwa wana virusi hivyo kaunti hiyo.

Robert Elim

Presenter and News Editor at North Rift Radio Kenya