Vijana kaunti ya Pokot Magharibi wameshauriwa kujihusisha na maswala ya siasa kwa kuwania viti mbali mbali ili nao waweze kuwa ndani ya serikali.
Kulingana na Katelem Josephat, kwa kipindi kirefu vijana wametumika vibaya na sasa ni zamu yao kujituma.
Aidha Katelem ameskitikia hatua ya baadhi ya wanasiasa kuwashinikiza Wakaazi Pokot Magharibi kuisoma ripoti ya mapendekezo ya BBI wakati wananchi hawajapata nakala ya ripoti hiyo.
Anasema itakuwa vigumu kwa mwananchi kuipigia kura ripoti asiyoielewa.