Zaidi ya wafanyibiashara 1000 wa chini na kati watanufaika na mahabara ya kisasa ya kufanyia uchunguzi itakayojengwa na Shirika la kukadiria ubora wa bidhaa nchini ,KEBS.
Kulingana na mkurungezi mkuu wa KEBS mstaafu Liutenant Colonel Bernard Njiraini ,mahabara hayo yatakayojengwa viungani mwa mji wa Nakuru, itapunguza gharama ya usafirishaji iliyotumika hapo awali kusafirisha baadhi ya bidhaa hadi Jijini Nairobi ili kufanyiwa uchunguzi.
Akizungumza kwenye kikao na gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui, , Njiraini pamoja na mwenyekiti wa bodi ya KEBS mhandisi Bernard Ngore, amesem ujenzi wa mahabara hayo katika Ukanda wa Bonde la Ufa, utasaidia uzalishaji wa bidhaa za hali ya juu.