Kiongozi wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi ametoa wito kwa Serikali kuangazia upya bei ya mafuta iliyotangazwa wikendi iliyopita.
Mudavadi anasema Wizara ya fedha inapaswa kutafuta mbinu za kukwamua uchumi wa taifa bila kuwaumiza Wananchi wenye kipato cha chini.
Ameongeza kuwa wizara ya kawi haipaswi kupandisha bei ya mafuta akisema ilivyo kwa sasa Mwananchi wa kawaida amekandamizwa pakubwa.