Kampuni ya sukari ya Mumias imeanza uzalishaji wa ethanol mara baada ya kampuni hiyo kufungwa kwa miezi miwili kufuatia kupungua kwa molasses.
Kufikia sasa kampuni hiyo imezalisha lita 150,000 ya Ethanol kwa awamu mbili ikiwa ni hatua kubwa kwa kampuni hiyo ambayo imekuwa ikipitia changamoto kwa takriban miaka miwili.
haya yanajiri huku kukiwepo na hitaji kubwa la virutubishi vya kutengeneza vyeyuzi ili kudhibiti msambao wa COVID-19 nchini.
Hata hivyo kampuni hiyo inahitaji shilingi nusu billioni kununua vyuma vipya ili kuendeleza uzalishaji wa sukari.