Kaunti ya ndogo ya Turkana ya Kati imeripoti visa 1,282 vya mimba miongoni mwa wasichana walio na umri mdogo kati ya mwezi Machi na Juni mwaka huu.
Afisa wa kituo cha Huduma kwa Vijana katika hospitali ya Rufaa ya Lodwar Virginia Ikal amesema kuwa hali hiyo inasababishwa na hatua ya kufungwa kwa shule kwa muda mrefu kutokana na athari za janga la virusi vya corona.
Aidha Ikal amesema baadhi ya wasichana walio na ujazito wana umri wa kati ya miaka 10 na 19 huku akisema vijiji vya Kanamker,Nawoitorong na Nakwamekwei vilivyoko viungani mwa mji wa Lodwar vimeripoti idadi ya juu ya wasichana waliopachikwa mimba wakiwa na umri mdogo.
Wakati huo huo Mshauri katika kituo cha vijana katika hospitali ya Rufaa ya Lodwar Bereta Onduu amewataka wazazi pamoja na washikadau kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita kukithiri kwa mimba za mapema na kuwapa nasaha njema watoto wao
Hata hivyo amesema ni muhimu hatua za haraka kuchukuliwa ili kukomesha tabia hiyo ambayo aliitaja kama dhuluma kwa wasichana wadogo kwani wengi wao wameambukizwa magonjwa ya zinaa.