Zaidi ya wanafunzi 1000 katika kaunti ya Turkana wamefaidika na vitabu, madawati na viti kutoka kwa wakfu wa safaricom.
Miongoni mwa shule zilizopokea vifa hivyo ni pamoja na shule ya msingi ya Katiko, Jeriman Lokitaung.
Kulingana na mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Nakiria, Eliud Aree shule ambayo ilifaidi na ujenzi wa maktaba anasema kwamba wananfunzi wamepoata motisha ya kusoma kwa bidii akiongeza kwamba idadi ya wananfunzi imeongezeka hata zaidi kutokana na mazingira bora ya wanafunzi kusomea.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa wakfu wa Zizi Afrique John Mugo anasema kwa ushirikiano na wakfu wa Safaricom wanalenga kuimarisha sekta ya elimu katika kaunti ya Turkana kwa kujenga maktaba kadhaa, kufadhili ujenzi wa madarasa vile vile kuwapa vitbu na vifaa vingine.