VIONGOZI WAKUU SERIKALINI WAENDELEA KUTUMA RISALA ZA RAMBIRAMBI BAADA YA KIFO CHA WAZIRI WA ZAMANI YUSUF HAJJI.

You are currently viewing VIONGOZI WAKUU SERIKALINI WAENDELEA KUTUMA RISALA ZA RAMBIRAMBI BAADA YA KIFO CHA WAZIRI WA ZAMANI YUSUF HAJJI.

Viongozi mbalimbali akiwemo Rais Uhuru Kenyatta wanaendeleo kutuma risala za rambirambi kwa familia ya seneta wa kaunti ya Garissa Yusuf Hajji ambaye amefarika alfajiri ya leo katika hospitali ya Aga Khan ambako amekuwa akipokea matibabu.

Kwa mujibu wa familia ya mwendazake amekuwa akiugua kwa muda na ndipo alipokutana na mauti yake asubuhi ya leo.

Hata hivyo Hajji anatarajiwa kuzikwa Alasiri ya leo katika makumburi ya kiislam ya Langat,jiji Nairobi.

Itakumbukwa kwamba Hajji amekuwa muhimili katika maadalizi ya Ripoti ya Upatinishi BBI katika wadhifa wa Mwenyekiti lakini pia aliwahi kuhudumu kama Waziri wa Usalama wa Ndani kati ya mwaka 2008-2013

Kifo cha Hajji kinajiri baada ya Waziri wa zamani wa Kenya Simon Nyachai kufariki wiki mbili zilizopita huku akitarajiwa kuzikwa leo baada ya mwili wake kuwasili jana nyumbani kwake kaunti ya Kisii.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa