Viongozi wa kidini katika kaunti ya Uasin Gishu wamelalmika kuhusu kile wamedai ni kudorora kwa uchumi wa taifa jambo ambalo wanasema limechangia pakubwa kudorora kwa maisha hivyo kuwafanya wakenya wengi wa mapato ya chini kuendelea kutaabika.
Wakiongozwa na imam katika msikiti wa Jua Kali Eldoret Ishmael Mohammed wanasema kupanda kwa bei ya chakula vile vile ada ya umeme imewafanya wengi kuhangaika na kushindwa na maisha ambayo wanasema yanaendelea kuwa magumu kila kukicha.