Serikali ya kaunti ya Pokot magharibi imeangazia zaidi kuweka dhamana katika bidhaa za maziwa kwa kuanzisha kiwanda cha maziwa katika eneo la Kabichbich Pokot kusini.
Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo la ujenzi wa kiwanda hicho gavana John Lonyang’apuo amelezea faidi nyingi ambazo wafugaji wa ng’ombe wa maziwa watapata kutokana na kilimo hicho.
Lonyang’apuo ametoa hakikisho kwa wakulima kwamba kiwanda hicho kitafungua mianya ya vijana wengi kupata ajira sawa na kuongezeka kwa bei ya maziwa.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na waziri wa kilimo Godfrey lipale ambaye anasema serikali inalenga kuhakikisha visa vya ufugaji wa kuhamahama inapunguzwa na kutoa nafasi kwa wakulima kukumbatia kilimo cha ng’ombe wa maziwa
Ameongeza kuwa malengo ya uongozi wa Gavana Lonyang’apuo inaenda sambamba na ajenda za utawala wa rais Uhuru Kenyatta kuhusu ustawishaji wa viwanda na kuinua viwango vya uzalishaji.