Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Vinka amedai kwamba likizo ya uzazi au ulezi haiwezi kumlisha hivyo amethibitisha kurejea tena kwenye shughuli zake za kimuziki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Vinka amepost baadhi ya picha akiwa anatumbuiza kwenye hafla ya harusi na kuthibitisha kwamba ameanza kufanya matamasha mbali mbali ya muziki ili aweze kujikimu kimaisha.
Kauli Vinka inakuja wiki moja baada ya kupewa likizo ya miezi sita kwa ajili kutoa malezi kwa mtoto wake lakini inaonekana amekaidi amri hiyo na kuanza kutumbuiza kwenye hafla mbali mbali ya harusi.
Ikumbukwe mwanamuziki huyo ambaye yupo chini ya lebo ya muziki ya Sony Music Entertainment hajeoneka mbele ya umma au kutumbuiza kwenye hafla yeyote kwa takriban mwaka mmoja.