CHAD JOHNSON: DRAKE NA RICK ROSS MBIONI KUJA NA ALBUM YA PAMOJA

You are currently viewing CHAD JOHNSON: DRAKE NA RICK ROSS MBIONI KUJA NA ALBUM YA PAMOJA
  • Post category:Burudani

Wakali wa muziki wa Rap, Drake kutoka Kanada na Rick Ross kutoka nchini Marekani wametajwa kuwa kwenye mpango wa ushirikiano wa album ya pamoja.

Taarifa za hizo zimethibitishwa na aliyekuwa mchezaji nyota wa Kikapu nchini marekani, Chad Johnson ambaye amevujisha taarifa za Drake na Rick Ross  kuwa kwenye mpango huo kupitia mtandao wa twitter.

Katika taarifa aliyovujisha Johnson, ameeleza kuwa album hiyo ya wakali hao itakuwa na ngoma kali kuliko kolabo zozote walizowahi kufanya mastaa hao kabla.

Hata hivyo mwaka 2021 Drake alishadokeza juu ya ujio wa album yake na Rick Ross iliyodai kuwa itaiwa ‘You Only Live Once’ na kusema ilicheleweshwa na matatizo ya kiafya aliyompata Rick Ross wakati huo.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa