Nyota wa muziki nchini Nadia Mukami ameshinda tuzo ya Zuri Awards mwaka wa 2021 kupitia kipengele cha Finance Category.
Nadia Mukami ameshare taarifa hiyo nzuri kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba ana furaha kushinda tuzo hiyo kupitia mpango wake uitwao Finance Discipline Journey.
Finance Discipline Journey ni mpango ambao Nadia Mukami alianzisha kwa ajili ya kuwahimiza vijana nchini kujenga tabia ya kuweka akiba.
Ikumbukwe Tuzo za Zuri Awards hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutoa heshima na kusherekea wanawake ambao wamebadilisha jamii kupitia njia mbali mbali za kimaendeleo.