Mara baada ya Naomi Campell kutangazwa kama balozi wa utalii nchini,wakenya wengi walihoji kwanini wizara ya utalii imchague Campell na sio muigizaji wa kimataifa Lupita Nyongo ambaye ana asili ya Kenya.
Waziri wa utalii nchini “Najib Balala” alijibu kwa kusema kuwa wizara yake ilijaribu kuwasiliana na Bi Nyong’o bila mafanikio kwa miaka mitano sasa.
Waziri Balala alisema “Najua kila mtu anajiuliza kwanini sio Lupita,Lupita anamakubaliano na menejimenti yake na mameneja wake hawakuturuhusu kumpata Lupita,ni kwa miaka mitano sasa tumekuwa tukimtafuta Lupita” hicho ndicho alichokisema Waziri Balala
Lupita Nyongo pia ameisikia kauli hii ya waziri na kuwaaminisha watu kuwa hakuwahi kutafutwa,alipost picha ambayo anacheka kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuandika “Mimi ninaposikia kuwa waziri wa utalii amekuwa akinitafuta kwa miaka 5”.
Kwa post hiyo ya Lupita huenda hakuwahi kupata taarifa za yeye kutafutwa na wizara ya utalii nchini Kenya.