Msanii wa muziki wa Bongofleva Lava lava ameachia rasmi EP yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.
EP hiyo inakwenda kwa jina la “Promise” Ina jumla ya nyimbo 4 huku akiwa amewapa mashavu wakali kama Diamond na Mbosso.
Promise EP ni kazi ya kwanza ya Lava lava kwa mwaka huu wa 2021 na ni maalum kwa ajili ya kuunogesha msimu huu wa Valentines huku ikisheheni nyimbo zenye jumbe za mahaba katika kuhakikisha wapendanao wanaonyeshana mapenzi shata shata.
Hata hivyo Promise EP inapatikana Exclusive kupitia platforms zote za kuuza na kuusikiliza muziki duniani ikiwemo Apple Music, Spotify, Boomplay miongoni mwa nyingine kibao.