Rapa kutoka Marekani Bow Wow anataka kuushtua ulimwengu kwa kutumia majina ya Wanawake aliowahi kutoka nao kimapenzi, kama majina ya nyimbo (tracklist) kwenye album yake ijayo.
Kwenye sehemu mpya ya kipindi cha Growing Up Hip Hop Atlanta, Bow Wow ametaja baadhi ya majina ya Wanawake hao akiwemo; Blac Chyna, Keyshia Cole na Angela Simmons.
Wiki iliyopita Bow Wow alidokeza kuachia album yake ya mwisho kabla ya kuacha muziki na ameipa jina ‘Before 30’