MENEJA WA ZAMANI WA SSARU AFUNGUKA SABABU ZA KUICHUKUA AKAUNTI YA YOUTUBE YA MSANII HUYO.

You are currently viewing MENEJA WA ZAMANI WA SSARU AFUNGUKA SABABU ZA KUICHUKUA AKAUNTI YA YOUTUBE YA MSANII HUYO.
  • Post category:Burudani

Aliyekuwa Meneja wa msanii Ssaru John Kennedy amefunguka kwa mara ya kwanza sababu za kuichukua channel ya mtandao wa Youtube ya msanii huyo.

Kupitia mitandao yake kijamii John Kennedy amesema Ssaru alianza kuingiwa na kiburi alipoanza kutoka kimapenzi na baadhi ya watangazaji maarufu nchini na alipojaribu kumshauri msanii huyo alimtukana matusi ya kila aina, jambo ambalo anadai lilimkasirisha na kusitisha kufanya kazi na ssaru.

Haikushia hapo alienda mbali zaidi na kusema kwamba alichukulia youtube channel ya msanii huyo ili aweze kurejesha pesa nyingi alizowekeza kwa Ssaru ikizingatiwa kuwa alikuwa ana gharamikia kila kitu ya msanii huyo kutoka kutayarisha muziki wake hadi kushoot video za nyimbo zake.

Hata hivyo amesema ana siri nyingi sana za Ssaru  ambayo amedai akiziweka wazi kwa umma huenda ikamharibia brand yake lakini kwa sababu bado anamjali hawezi fanya hivyo licha ya msanii huyo kumfokea na kumtusi akiwa nyumbani kwake.

Ikumbukwe Ssaru kwa sasa ana amefungua akaunti nyingine ya youtube baada ya aliyekuwa meneja wake John Kennedy kuichukua akaunti yake iliyokuwa na takriban suscribers  78,000.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa