Mwanamuziki anayesuasua kwenye kiwanda cha muziki nchini uganda Angela Katatumba amedai kuwa wasaniii wengi nchini humo wana uelewa mdogo kwenye masuala ya muziki kwani hawajasafiri maeneo mbali mbali ulimwengu.
Akipiga stori na Voice of Africa, hitmaker huyo wa ngoma ya “Tonelabira” amesema imefika wakati wanamuziki wa uganda waache kuwa na mawazo finyu kwenye muziki wao na badala yake wajifunze kutoka kwa wasanii waliofanikiwa kutoka maeoneo mengine duniani.
Hata hivyo Angela Katatumba amesema suala la wasanii kutegemea soko la uganda pekee limepelekea wengi wao kutoa muziki duni ambao haujakamilika kwa sababu hawajapata msukumo wa kufanya muziki mzuri