Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee ameachia rasmi album yake mpya iitwayo ’20’.
Lady Jaydee ambaye ni moja kati ya wasanii waliyoupa muziki wa Tanzania thamani, ameachia album yake hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 20 ya uwepo wake kwenye kiwanda cha muziki wa Bongofleva.
Album hiyo inayopatikana kwenye platforms mbalimbali za kusambaza muziki duniani, ina jumla ya nyimbo 20 zilizobeba uandishi wenye ujumbe na burudani.
Hata hivyo, Jaydee anaachia album yake hii ya nane ikihesabika kuwa tayari ameutumikia muziki nusu ya umri wa maisha yake mpaka sasa.