Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametangazwa na waandaji wa tuzo za muziki za MTV Mama 2021 kama mmoja wa wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo.
Orodha ya wasanii watakaotumbuiza katika tuzo hizo za kimataifa ambazo kwa msimu huu zitafanyika Februari 20 nchini Uganda kwa njia ya kidigitali ilitolewa Januari 27 ikiwa na wasanii nane kutoka nchi nane tofauti ya Afrika.
Aidha majina ya wasanii nane yaliyojitokeza kwenye orodha ya watumbuizaji hao ni Diamond (Tanzania), Nasty C (Afrika Kusini), Soraia Ramos (Cape Verde), Khaligraph Jones (Kenya), Sheeba (Uganda), WizKid (Nigeria), Suspect 95 (Ivory Coast) na kundi la Calema kutoka Sao Tome.
Mbali na kuchaguliwa kutumbuiza, pia Diamond anawania tuzo hizo pamoja na wasanii wengine 7 kutoka Tanzania ambao ni Harmonize, Zuchu na kundi la muziki wa Hip Hop la Rostam.
Tuzo za MTV Mama hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kuwatunuku wasanii wa Afrika waliofanya vizuri kisanaa kwenye mwaka husika, na safari hii itakuwa ni mara ya kwanza kufanyika nchini Uganda.