Hatimaye Bulldog mbili za Kifaransa za Nyota wa muziki kutoka Nchini Marekani Lady Gaga zimepatikana salama mwishoni mwa juma lilopita baada ya kuibiwa,
Mbwa hao wawili koji na Gustav waliibiwa Jumatano usiku wiki iliyopita baada ya mtu mwenye bunduki kumpiga risasi Ryan Fisher aliyekuwa akiwatembeza mbwa hao huko Los Angeles
Lady Gaga alikuwa ameahidi kutoa shillingi millioni 5.4 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa Bulldogs hao
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na polisi wa Los Angeles mwanamke mmoja ambaye jina lake halijatajwa ndiye aliwapeleka kituoni hapo, na inaonekana mwanamke huyo “hajahusika na hana uhusiano wowote” na shambulio hilo.
Bado Hakuna Taarifa nyingi juu ya jinsi mwanamke huyo aliwapata mbwa hao, lakini hivi karibuni atakuwa tajiri wa shillingi millioni 5.4 kwani Lady Gaga atakuwa amefurahi na kufarijika sana baada ya kupatikana kwa Bulldogs hao.