CHOZEN BLOOD ACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA “AM CHOZEN”.

You are currently viewing CHOZEN BLOOD ACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA “AM CHOZEN”.
  • Post category:Burudani

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Chozen Blood hatimaye ameachia rasmi album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.

Album hiyo ambayo ameipa jina la “Am Chozen” ina jumla ya ngoma 11 za moto huku, akiwa na ameshirikisha wasanii mbali mbali nchini uganda akiwemo John Blaq, na Fik Fameica.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Chozen Blood ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa “Sharp Shooter”  amewashukuru maprodyuza waliosimamia  mchakato wa kuitayarisha album hiyo na hatimaye kuitoa.

Album ya “Am Chozen” inapatikana ‘exclusive’ kupitia mitandao yote ya kukisikiliza na kuuza muziki duniani kama vile Boomplay, Spotify na Apple Music.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa