Wiki moja iliyopita aliyekuwa mpenzi wa msanii King Saha, Joweria Ali alimshauri msanii huyo aache kutumia mihadarati la sivyo huenda akapoteza maisha yake.
Hii ni baada ya picha ya king saha kusambaa mitandaoni ikimuonyesha amedhofika kiafya na kuibua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Sasa kwenye moja ya Interview King Saha amemshauri aliyekuwa mpenzi wake huyo atafute kitu cha kufanya na amsahau kabisa katika maisha yake.
Kulingana na King Saha, anajali sana maisha yake kuliko ya mpenzi wake huyo wa zamani,hivyo hana ruhusa ya kukumbusha kitu cha kufanya katika maisha.
Ikumbukwe mwaka mmoja uliopita, msanii bebe cool alimshauri king saha aachane na suala la kutumia dawa za kulevya kabla ya hajepoteza mweelekeo kwenye shughuli zake za muziki.