Aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ametoa msamaha kwa wasanii nyota wa muziki wa Rap nchini humo, Lil Wayne na Kodak Black katika siku yake ya mwisho ofisini.
Trump ametoa msamaha kwa watu zaidi ya 100 wakiwemo nyota hao kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu wa waandishi wa habari wa Ikulu ya White House nchini humo, Kayleigh McEnany usiku wa kuamkia leo.
Lil Wayne alikuwa akikabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 gerezani baada ya kukiri kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria wakati wa akisafiri kwa ndege binafsi mnamo Desemba 2019.
Kodak Black, ambaye jina lake halisi ni Bill Kapri, alihukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka mitatu gerezani Novemba 2019 kwa kosa la kughushi Nyaraka ili kupata silaha
Biden na Makamu wake Kamala Harris wameapishwa rasmi Jumatano (Januari 20), Biden anakuwa Rais wa 46 wa Marekani Baada ya kuibuka Mshindi wa Uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba mwaka jana.