DR DRE ADAIWA KUMTELEKEZA BABA YAKE MZAZI.

You are currently viewing DR DRE ADAIWA KUMTELEKEZA BABA YAKE MZAZI.
HOLLYWOOD, CALIFORNIA - FEBRUARY 07: Dr. Dre attends the Tom Ford AW20 Show at Milk Studios on February 07, 2020 in Hollywood, California. (Photo by Mike Coppola/FilmMagic)
  • Post category:Burudani

Misukosuko inazidi kumuandama Mtayarishaji nguli wa muziki duniani Dr. dre . Ikiwa ni siku chache zimepita toka aripotiwe kulazwa ICU baba yake mzazi Dr Dre anayefahamika kwa jina la Theodore Young ameibuka na kuweka wazi kuwa ametelekezwa na mtoto wake huyo.

Baba mzazi wa Dre amesema kuwa mara ya mwisho kuonana na mtoto wake huyo ilikuwa kwenye mazishi ya bibi yake na ni muda mrefu umepita wamekuwa hawana mahusiano mazuri kati yao.

Mzee Theodore Young ameiambia Page Six kuwa baada ya kuachana na mama yake Dr Dre Verna Dr Dre alichukuliwa na kwenda kuishi na Bibi yake pamoja na mama yake. Huko ndiko alikojazwa sumu juu ya baba yake jambo ambalo limesababisha mpaka leo kufungiwa vioo na Bilionea huyo.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa