Member wa kundi la Boondocks gang Exray amejitokeza kwa mara ya kwanza na kuzungumzia ishu ya kujiondoa kwenye kundi hilo ambalo linafanya vizuri na muziki wa gengetone.
Hii ni baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amejitoa kwenye kundi la Boondocks gang baada ya kuonekana akizitoa kazi zake kama msanii wa kujitegemea .
Akiwa kwenye moja ya Interview Exray amekanusha madai ya kujiondoa kwenye kundi hilo huku akisema hatua ya kuachia nyimbo kama msanii wa kujitegemea hainamaanishi kwamba amejiondoa kwenye kundi la Boondocks kwani ni njia moja ya kutanua wigo wa muziki wake.
Sanjari na hilo amekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba muziki wa Gengetone utakufa kwa kusema kwamba muziki huo bado una mashabiki waaminifu ambao ni wa asili ya kikenya.
Ikumbukwe Exray ni muasisi wa kundi la Boondocks gang ambalo lina wasanii kama Madoxx na Odi wa murang’a na lilipata umaaarufu nchini mwaka wa 2019 lilipoachia single iitwayo “Rieng”.