BAHATI AAHIDI KUWASHIRIKISHA MA VIDEO VIXEN WAFRIKA KWENYE NYIMBO ZAKE.

You are currently viewing BAHATI AAHIDI KUWASHIRIKISHA MA VIDEO VIXEN WAFRIKA KWENYE NYIMBO ZAKE.
  • Post category:Burudani

Staa wa muziki nchini Kevin Bahati amemjibu shabiki yake ambaye alimshtumu kwa hatua ya kuwatumia wanawake weupe kwenye video za nyimbo zake.

Shabiki huyo aliyefahamika kama Angila alicomment kwenye picha ya Bahati akiwa na video Queen wa wimbo wake  mpya uitwao Mi Amor na kuambia msanii huyo aendelee kuwatenga ma video Queen wanaotoka jamii ya watu weusi licha ya kwamba wanampenda.

Bahati alijibu comment ya shabiki wake huyo  kwa kutoa wito kwa ma Video Queen kutoka jamii ya watu weusi kumtumia ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kama wangependa awashirikishe kwenye wimbo wake ujao.

Ikumbukwe Bahati ni mmoja kati ya wasanii ambao walianza muziki kama waimbaji wa nyimbo za injili  lakini alikuja akaigura kiwanda cha muziki injili nchini kwa madai kwamba kiwanda hicho kimejaa chuki.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa