Pamoja na kutokuwepo kwa maelewano mazuri kati yao Staa wa mzuiki wa Bongo Fleva na Mkurugenzi wa WCB na Wasafi Media Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa Q Chief ndiye msanii wake bora wa muda wote na wimbo wa Nitampata Wapi ndio wimbo wake bora wa muda wote
Diamond amepost video kupitia Insta Story yake kwenye mtandao wa Instagram akiuangalia na kuimba wimbo huo kisha kuandika “Wimbo wangu bora wa muda wote, msanii wangu bora wa muda wote haijalishi kimetokea nini”
Wawili hao hivi karibuni walikuwa na vuta nikuvute baada ya Q Chief kulalamika picha yake na jina lake kutumika kwenye tangazo la wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha la tumewasha Tour Jijini Dar es Salaam huku akiwa hajafanya mazungumzo yeyote ya kibiashara na waandaaji wa Tamasha hilo.