RAPA BOBBY SHMURDA AFUNGUKA SABABU ZA KUKATAA KILEVI KWENYE VIDEO INAYOSAMBAA MITANDAONI.

You are currently viewing RAPA BOBBY SHMURDA AFUNGUKA SABABU ZA KUKATAA KILEVI KWENYE VIDEO INAYOSAMBAA MITANDAONI.
  • Post category:Burudani

Rapa  kutoka nchini Marekani Bobby Shmurda amefunguka sababu iliyomfanya kukataa kinywaji ambacho alipewa na mrembo mmoja alipokuwa club wikendi iliyopita. 

Kwenye video iliyonaswa Jumamosi hii iliyopita, Shmurda alionekana akikataa kinywaji ambacho kilitajwa kuwa kilevi kuepusha lolote baya akilewa

Sasa kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shmurda aliyetoka jela wiki iliyopita aliwaambia wafuasi wake kwamba bado yupo chini ya uangalizi wa bodi ya misamaha kwa wafungwa (parole board) hivyo hataki kujihusisha na mambo ya kihuni.

Mkali huyo ambaye alitoka kimuziki mwaka wa 2014, alihukumiwa kifungo cha miaka 7 Jela mwaka 2016 kwa kuhusishwa na kosa la mauaji. Februari 23 mwaka huu aliachiwa huru na ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa Bodi ya misamaha kwa wafungwa (Parole Board) hadi Februari 23 mwaka wa 2026.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa