Kundi la muziki nchini Sauti Sol limewaacha mashabiki wao na maswali mengi baada ya kupost picha ya pamoja na msanii wa Bongo fleva Juma Jux.
Kupitia ukurusa wao wa instagram sauti sol wamepost picha wakiwa na Juma Jux kwenye mazingira ya studio yenye caption inayoashiria kuwa kuna uwezekano wa kundi hilo kufanya wimbo wa pamoja na msanii huyo wa bongofleva.
Iwapo Sauti Sol watafanikisha mpango wa kufanya collabo na Juma Jux watakuwa wasanii wa pili kufanya kazi na msanii huyo baada ya Otile Brown ambaye tayari ana wimbo nae uitwao “Regina.”