Msanii wa nyimbo za injili nchini Ringtone amethibitisha kukataa tamaa kwenye ndoto yake ya kumiliki gari aina ya BMW i8.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ringtone ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa “Omba” amesema maombi yake hayajejibiwa ila amesema kwamba hatagura kiwanda cha muziki wa injili kama alivyotangaza kwa sababu Mungu amemfanyia mambo makubwa ambayo mpaka sasa yamemweka kwenye ramani ya muziki.
Sanjari na hilo Ringtone amekiri kununua ndege aina ya Helicopter ambayo imewashangaza wengi ikizingatiwa kuwa ndege hiyo ni ghali mno ikilinganishwa na gari aina BMW i8.
Ikumbukwe mapema mwaka huu Ringtone alitangaza kuwa ataacha muziki wa injili kama mungu atajibu maombi yake ya kumiliki gari aina BMW i8.