Nguli wa muziki wa Rap kutoka Nchini marekani ‘Dwayne Michael Carter, Jr’. Maarufu kama Lil Wayne ametangaza ujio wa album ya pamoja itakayo wajumuisha wasanii wote waliopo chini ya record label ya Young Money Entertainment.
Lil Wayne amethibitisha ujio wa Album hiyo wiki hii katika mahojiano yake na Fox Sports Radio Show , Nguli huyo amesema kuwa wamepanga kuanza na kazi ya pamoja kisha baadae ndipo msanii mmoja mmoja atatoa kivyake.
Bado Haijajulikana ni lini Album hiyo itaingia sokoni lakini itakua ndio album ya kwanza ya pamoja ya wasanii wa lebo hiyo tangu ifanye hivyo mwaka 2014 walipoachia Album ya ‘Rise of an Empire’