Mchekeshaji wa humu nchini Elsie Majimbo amekava Jarida la Teen Vogue toleo la mwezi machi mwaka huu.
Majimbo ambaye yupo nchini mMarekani kwa sasa hakuficha furaha yake kwani alitumia mitandao yake ya kijamii kwa hatua hiyo kubwa maishani huku akimshukuru mungu kwa kumpigania licha ya watu kwenye mitandao kumbeza.
Kwa matokeo hayo, baadhi ya wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kufurahia mafanikio aliyoyapata ambapo wengi wampongeza mrembo huyo kwa hatua hiyo kubwa maishani kwani sio jambo rahisi kwa mtu kutoka afrika kukava jarida la Teen Vogue.
Ikumbukwe Jarida la teen vogue ni jarida ambalo hutoka mara 12 kwa mwaka yaani mara moja kila mwezi na husisha watu mashuhuri pamoja na tasnia ya mitindo na Fasheni.