Msanii nguli wa muziki wa hiphop kutoka nchini Marekani The Game ameibuka na kujibu tuhuma za kuwatapeli wasanii wachanga wa Hip Hop.
Kwenye mahojiano na mtandao wa Hip Hop DX, The Game amesema tuhuma hizo hazina mashiko kabisa kwani adhma yake ni kusaidia vijana wachanga waweze kufanikiwa kimuziki.
Wiki hii zilitoka taarifa kwamba The Game amewatapeli rappers wachanga kwa kuwafata kwenye mitandao ya kijamii na kuwasifia kwa kazi nzuri, na baadaye kuwatoza pesa kwa makubaliano ya kupandisha ngoma zao kwenye akaunti yake ya SoundCloud na kutengeneza Compilation Album.
Baadhi ya wasanii hao walikuja hadharani na kusema The Game amewatapeli kwa kuwatoza takriban shillingi laki moja lakini hajatimiza ahadi zake.