SPICE DIANA ADAI HANA MPANGO WA NDOA.

You are currently viewing SPICE DIANA ADAI HANA MPANGO WA NDOA.
  • Post category:Burudani

Msanii anayefanya vizuri kwenye muziki nchini Uganda, Spice Diana, amesema moja ya vitu vinavyomtatiza kwa sasa ni kufanya maamuzi ya kuingia kwenye ndoa kwa kuwa bado wakati wake.

Mrembo huyo wa ngoma ya “Kokonya” amesema, kwa sasa anajipanga kwanza kwa ajili ya kuyaweka maisha yake kwenye mstari, hivyo hawezi kufikiria masuala ya ndoa.

Spice Diana amedai kuwa hataki kutegemea pesa za mume wake mtarajiwa na ndio maana ameelekeza nguvu zake zote kwenye suala la kusaka hela.

Hata hivyo amesema hana mpango wa kumpata mtoto kwa sasa hadi pale atakapokuwa sawa kiuchumi kwani anaamini kwamba itamsaidia kumlea mwanae bila changamoto yeyote.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa