Msanii wa muziki kutoka Uganda Kalifah Aganaga anazidi kumtolea uvivu kinara wa chama ha kisiasa cha NUP, Bobi Wine.
Akipiga stori na runinga moja nchini Uganda Kalifah Aganaga amesisitiza kuwa Bobi Wine ana ubinafsi mwingi na hajawahi watakia mazuri wanamuziki wengine.
Mkali huyo wa ngoma ya “Kiboko” ameenda mbali zaidi na kudai kuwa kushindwa kwa Chameleone kwenye kinyang’anyiro cha umeya wa jiji la Kampala kulichangiwa na Bobi Wine ambaye alimnyima bosi huyo wa lebo ya muziki ya Leone tiketi ya chama cha NUP.
Ikumbukwe Jose Chameleone alishindwa vibaya na Erias Lukwago aliyepo madarakani kwa sasa kwenye uchaguzi wa umeya wa jiji la Kampala ambao ulikuwa na ushindani mkali.