CHRIS BROWN AMJIBU VIBAYA SHABIKI AMBAYE ALILINGANISHA UWEZO WAKE NA NYOTA WA MPIRA WA KIKAPU NCHINI MAREKANI BEN SIMMONS.

You are currently viewing CHRIS BROWN AMJIBU VIBAYA SHABIKI AMBAYE ALILINGANISHA UWEZO WAKE NA NYOTA WA MPIRA WA KIKAPU NCHINI MAREKANI BEN SIMMONS.
  • Post category:Burudani

Msanii wa RnB kutoka Marekani Chris Brown hataki jina lake na uwezo wake ulinganishwe na mtu yeyote hapa duniani.

Hii ni baada ya kumjibu kwa maneno makali shabiki mmoja ambaye alilinganisha uwezo wake na mchezaji wa NBA, Ben Simmons.

Shabiki huyo aliandika kupitia mtandao wa Twitter kwamba Chris Brown na R&B yake ni kama Ben Simmons kwenye mpira wa Kikapu. Yani hakuna maendeleo yoyote wala hatua anayopiga, hashuki, yuko vile vile, ni msanii wa hovyo tu.

Chris Brown alishindwa kujizuia na kuamua kumshushia maneno makali shabiki huyo akitaka asimchezee hata kidogo na asimlinganishe na mtu yeyote. Kubwa zaidi alimwambia “Sasa nenda kamuulize mama yako, yupi ni baba yako halisi.” 

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa