Baadhi ya wadau wa muziki nchini wamemtolea uvivu Staa wa muziki nchini Otile Brown mara baada ya msanii huyo kumshirikisha mwanadada maarufu mitandaoni aitwaye Shakilla kwenye wimbo wake mpya uitwao “Go Down.”
Licha ya single hiyo kupokelewa kwa uzuri na wapenzi muziki mzuri nchini inaonekana kuna baadhi ya watu ambao hawajefurahishwa na hatua ya Otile Brown kumtumia shakilla kama video vixen kwenye wimbo wake huo.
Sasa kupitia mitandao ya kijamii baadhi ya mashabiki wameonekana kumshambulia Otile Brown huku wakisema kwamba msanii huyo hakufanya vizuri kumshirikisha mrembo huyo kwenye wimbo wake wa “Go Down” kwani uwepo wake hauna mashiko kwenye video ya wimbo huo.
Ikumbukwe tangu mwanadada Shakilla apate umaarufu nchini kupitia mitandao ya kijamii wakenya wengi hajewahi furahishwa na mienendo yake kutokana na vituko vyake ambavyo wengi wanahisi kwamba vinakwenda kinyume na maadili ya jamii.