MR SEED AMTAKA RINGTONE APOKO AKOME KUWAHUKUMU WASANII WENZAKE WANAOFANYA MUZIKI WA INJILI.

You are currently viewing MR SEED AMTAKA RINGTONE APOKO AKOME KUWAHUKUMU WASANII WENZAKE WANAOFANYA MUZIKI WA INJILI.
  • Post category:Burudani

Msanii wa muziki wa Injili nchini Mr Seed amemjibu mwimbaji aliye na utata nchini Ringtone Apoko, akimwomba ajitenge na suala la kuwahukumu wasanii wengine, hii ni baada ya kuzungumza vibaya juu ya collabo yake ijayo na kikundi cha Gengetone cha Sailors.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Ringtone Apoko alimsuta vikali Mr Seed ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa lebo ya Starborn Empire, akimshutumu kwa kupotosha tasnia ya muziki wa injili nchini kwa hatua ya kushirikiana na wasanii wa kidunia.

“Acha upuuzi huu  mr seed, nenda kwa muziki wa kidunia. wimbo wako wa kijinga unaotaka kuuachia, Wakristo hawataupokea. Bure kabisa takataka ”Sauti ya Ringtone kwa Mr Seed ilisikika.

Hata hivyo  Mr Seed alishindwa kuvizuia vidole vyake na kuamua kumshushia maneno makali Ringtone  Apoko akimtaka aache kuhukumu, kwa kusema kuwa hakuna mtu aliye mwadilifu na ni Mungu tu anayeweza kuhukumu.

“…industry ya gospel imekuwa na issues, tumekuwa na a lot of judging badala ya ku support, fighting badala ya kusupport. Mtu akitakuchnage akuwe a gospel artiste tunamjudge badala ya kumsikiza tunamjudge, ambayo sio sawa. Sisi sio Mungu. Hatutakiwi kumhukumu mtu yeyote na uamuzi yenye amemake. …

For me ku support Lexy from Sailors venye ameamua kufanya gospel imekuwa tena shida. Rafiki yangu wewe sio Mungu. Kwanza kabisa, Mungu hakuja kwa ajili ya kanisa, Mungu alikuja kwa wale watu hawamjui, wewe unamjua ni sawa, lakini acha kuhukumu wengine, acha kupigana na wengine, sio sawa ”amesema mr seed.

Kauli ya mr Seed inakuja wakati member wa sailors gang Lexy Yung amehamia kwenye muziki wa Injili,huku akionekana kumuomba msamaha Mwalimu Rachel na KRG the Don kufuatia mzozo wao mwaka jana.

 “Samahani mabro kwa hili .. Na ni kwa machozi mengi Bana ..tumekuwa pamoja nimefanya mengi na kufanikisha mengi mih l wish you all best in your journey. Mih nmeamua kufanya muziki wa injili sitawainamisha uko. Nahidi kuwa migongo mwenu. WASANII WA INJILI HAPA NAJA …… ”alipost Lexy Yung kwenye mitandao yake ya kijamii.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa