Bifu la Rapa Tekashi 69 na Meek Mill kutoka nchini marekani linaendelea kushika kasi, Tekashi ameibuka na madai kwamba Meek Mill ametuma barua kwa Wanasheria wake akidai kuwa anafanyiwa vitendo vya uonevu (Bullying)
Kwenye barua hiyo iliyowekwa na tekashi 69 kwenye mtandao wa instagram, inamkataza tekashi kuacha kutumia video na picha za Meek Mill kwa lengo la kujinufaisha kibiashara.
Kwenye video ya wimbo wake mpya uitwao “ZAZA” rapa Tekashi amemdhihaki Meek Mill kwa kutumia picha yake pamoja na video inayoonesha wakizozana, bila ridhaa yake.
Hivyo wanaomba kipande hicho kilichoanzia sekunde ya 50 kuondolewa mara moja kwenye video hiyo ambayo tayari ina zaidi ya viewers millioni 29 kwenye mtandao wa YouTube.