Baada ya kuufungua mwaka wa 2021 vizuri na wimbo wake wa “Infidele”, Boss wa lebo ya muziki ya Kings Music Ali Kiba ameweka kambi nchini Nigeria mapema wiki hii ambapo atakaa kwa muda wa wiki mbili
Alikiba ameweka bayana hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika “Lagos for 2 weeks, Album almost done”.
Album ya Alikiba mpaka sasa haijafahamika itaitwaje na itatoka rasmi mwezi gani japo tetesi zinasema kwamba itatoka mwezi April mwaka huu wa 2021 na itakuwa na nyimbo si chini ya 20.