T.I. NA MKEWE WAKANUSHA TUHUMA ZA UNYANYASAJI WA KINGONO.

You are currently viewing T.I. NA MKEWE WAKANUSHA TUHUMA ZA UNYANYASAJI WA KINGONO.
  • Post category:Burudani

Rapa kutoka Marekani T.I. na mkewe wamevunja ukimya wao na kukanusha tuhuma za unyanyasaji wa kingono zilizotolewa na wanawake zaidi ya 25 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Rapa huyo ametumia njia ya video kuzungumzia suala hilo ambapo amesema tuhuma hizo ni  za uongo na hazina ukweli wowote. 

“Kwa nguvu zote na hekima tunakanusha tuhuma hizi za kipuuzi zilizotolewa na watu wasiofahamika.” ilisomeka caption kwenye video hiyo yenye dakika 8.

T.I. ameendelea na kusema kwamba ilikuwa ngumu kuweza kukaa kimya kufuatia tuhuma hizo ambazo pia zinamchafua na mkewe Tiny Harris. 

Hata hivyo anaamini amechafuliwa jina kwa sababu wanaomtuhumu hawajafungua shauri lolote mahakamani.

“Hatujawahi kumlazimisha mtu yeyote, hatujawahi kumuhusisha mtu yeyote kwenye masuala ya kingono, hatujawahi kumteka mtu yeyote pasina ridhaa yake. Hatujawahi kusafirisha chochote, yani kinachohusu biashara ya ngono.” alisema T.I. na kukanusha pia tuhuma za kubaka, “Sijawahi kumbaka mtu yeyote, kamwe sijawahi kumbaka yeyote.”

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa