Wasanii kutoka jamii ya Karamoja nchini Uganda wameshtumu vikali staa wa muziki nchini humo Bebe Cool kwa madai ya kuwapa ahadi ya uongo.
Kwa mujibu Evy Trey mmoja wa wasanii kutoka Karamoja Bebe Cool aliwagiza watumie pesa zao kurekodi nyimbo za kampeini kwa ajili Rais Yoweri Museveni na baadae watalipwa gharama zote walizozitumia kwenye suala la uandaaji wa nyimbo hizo lakini mpaka sasa hawajepokea pesa zozote.
Hata hivyo Juhudi za Jarida la Press Time nchini uganda kumtafuta bebe cool azungumzie suala hilo hazikuzaa matunda kwani simu zake zote zilikuwa zimezimwa.
Kauli ya wasanii hao inakuja siku chache baada ya msanii chipukizi nchini uganda aitwaye Zulunda kujitokeza na kumsuta vikali bebe cool kwa madai kwamba alikimbia na pesa zake kupitia wimbo wa mwongedde Akululu aliomuandikia msanii huyo kwa ajili ya kampeini za uchaguzi uliopita nchini Uganda.