Msanii wa muziki nchini Pascal Tokodi ambaye pia ni muigizaji amewatolea uvivu wanaomkashifu baada ya kuwambia Rais Uhuru Kenyatta atazame kipindi chake cha Selina kwenye moja ya video inayosambaa mitandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Tokodi amesema hajutii kumwambia Rais afutilie kipindi cha Selina ambacho kinaruka kupitia runinga Maisha Magic East huku akisema hatotisha na maneno ya watu mitandaoni kwani alihamua kuzitumia sekunde 15 alizokutana na rais kenyatta kujitetea kuhusiana na shughuli yake ya uigizaji.
Kauli yake inakuja mara baada ya watu kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii kwa kushindwa kumuuliza Rais Uhuru Kenyatta masuala muhimu ambayo kwa njia moja au nyingine yangemsaidia kimaisha.