Nyota mpya wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzani Anjella ambaye kwa sasa anasaidiwa na msanii harmonize kwenye upande wa muziki na matibabu, ameeleza kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa miguu ambao ulimuanza tangu akiwa darasa la 7.
Anjella amesema amepambana sana na ugonjwa huo mpaka wakakata tamaa wakabaki kufanya maombi ila anamshukuru Harmonize ambaye ameahidi atamsaidia na kumpeleka nchini India.
Nyota huyo mpya wa muziki wa Bongofleva, kwa sasa ameingia rasmi mjini kupitia wimbo mpya alioshirikishwa na msanii Harmonize uitwao “All Night”.